Kiu

I'm Building My House (Swahili)

Written by Lenny Smith and Steve Israel
Links to contributors: Steve Israel, Lenny Smith, Grace & Glory Singers, Lenny's Substack

The Grace & Glory Singers in Kenya translated and sang this song in Swahili. It sounds great! - July 18, 2023

Languages for this song:
English, Italian, Swahili



Lyrics

Ninayo makao kando kando ya mto
Maji yatiririka usiku mchana
Nikiwa na kiu huenda kando ya mto
Kisha nakata kiu kwa raha zangu

Mimi sina kiu tena, mimi sina kiu tena
Nayanywa maji ya uzima
Mimi sina kiu tena, mimi sina kiu tena
Nayanywa kwa raha zangu

Ni mengi makao kando kando ya mto
Maji yatiririka usiku mchana
Nakukaribisha hapa kando ya mto
Kisha tukate kiu kwa raha zetu

Sisi hatuna kiu tena, sisi hatuna kiu tena
Twayanywa maji ya uzima
Sisi hatuna kiu tena, sisi hatuna kiu tena
Twayanywa kwa raha zetu

Kama umechoka hujui uende wapi
Kukata kiu cha moyo
Njoo kwenye mto wa maji ya uzima
Moyo wako na upone

Ni mengi makao kando kando ya mto
Maji yatiririka usiku mchana
Nikiwa na kiu huenda kando ya mto
Kisha nakata kiu kwa raha zangu

Mimi sina kiu tena, mimi sina kiu tena
Nayanywa maji ya uzima
Mimi sina kiu tena, mimi sina kiu tena
Nayanywa kwa raha zangu

Sisi hatuna kiu tena, sisi hatuna kiu tena
Twayanywa maji ya uzima
Sisi hatuna kiu tena, sisi hatuna kiu tena
Twayanywa ka raha zetu
Twayanywa kwa raha

Copyright © 1997 New Jerusalem Music
Translation by Grace and Glory Singers

Comments -  Leave a comment